Promoting the rights of domestic workers ,and children and youths living and working in the streets
03 September, 2021
Source : News

Leo tarehe 3/9/2021 ofisi yetu, WoteSawa, imepokea ugeni kutoka Legal Services Facility (LSF) ambao ni wafadhili wetu katika mradi wa "Kuhamasisha Upatikanaji wa Haki kwa Wafanayakazi wa Nyumbani na Watoto na Vijana Wanaoishi na Kufanyakazi Mtaani kupitia uwezeshwaji wa Kisheria." Lengo la ugeni huu ni kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa mradi. LSF waliambatana pia na shirika la Railway Children Africa, ambao ni washiriki wetu katika kutekeleza mradi huo.

LSF, Railway Children Africa, na WoteSawa walitembelea maeneo ya mradi katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana na kuongea na walengwa wa mradi.