Shirika la WoteSawa domestic workers
23 May, 2020
Author : Wotesawa
Source : News
Tarehe 23/05/2020 siku ya jumamosi,Shirika la WoteSawa domestic workers lilitembelea maeneo mbalimbali katika viunga vya Jiji la Mwanza na kukutana na baadhi ya Wanawake wanao fanya kazi ndogondogo (vibarua) na Wafanyakazi wa Ndani. (na hapa ni maeneo ya libert)

Wanawake hawa walio wengi ni watu wa zima na wanafamilia zinazo wategemea pamoja na kipato chao kidogo kinacho tokana na kufanya kazi za ndani.

Huamka asubuhi na mapema kuelekea katika maeneo yao ya kazi za ndani ambazo ni pamoja na Kufua, Kufanya usafi wa ndani ya Nyumba na mazingira yote kwa ujumla.

Ni kweli wana taarifa juu ya ugonjwa huo ingawa kwa kiasi kidogo sana, kwa sababu wanawake hao tulionanana nao wote 52 walikuwa hawajavaa barakoa wala kuwepo kwa ndoo yenye maji ya kunawa au kuwa na vitaksa mikono. Hivyo tuliwagawia wanawake hao barakoa na vitakasa mikono. Walishukuru na kutusisistiza tuzidi kuwatembelea kwani wanazo changamoto nyingi sana ambazo wangependa kusaidiwa wapate ufumbuzi. 
"Kwa sasa kazi zimepungua maana watu wengi wamejifungia ndani na hivyo kusababisha tukose kazi nyingi na hivyo kukosa ipato cha kila siku" 
…! tuwafikie watanzania bila kuchoka.