EMAIL US AT info@wotesawa.or.tz
CALL US NOW +255-282-500-599
DONATE NOW

Wafanyakazi Wa Nyumbani Jijini Mwanza Wafurahia Mafunzo Ya Afya Ya Uzazi.

Wafanyakazi wa nyumbani wapatao 5o Jijini Mwanza wameyapokea kwa furaha mafunzo ya afya ya uzazi, yanayotolewa na Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WoteSawa.

Mafunzo hayo yalianza jana Januari 18 2018 katika ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza na yanatarajiwa kufikia tamati kesho ambapo washiriki wa mafunzo hayo wanajengewa uelewa zaidi juu ya afya ya uzazi na utambuzi ili kuondokana na changamoto wanazoweza kukumbana nazo ikiwemo mimba za utotoni na magonjwa ya zinaa.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa WoteSawa,�Afisa Miradi wa shirika hilo�Veronica Rodrick alisema mafunzo hayo yatawasaidia kujitambua na hivyo kutimiza vyema majukumu yao ya kazi.

Wakufunzi wengine wa mafunzo hayo, Jenifer Nelson ambaye ni Mratibu wa Vikundi vya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WoteSawa pamoja na�Renalda Mambo ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii WoteSawa, walihamiza wafanyakazi hayo kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati na kuwahimiza kufikisha elimu waliyoipata kwa wenzao.

Mkufunzi mwingine, Demitila Faustine ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii WoteSawa alisema mafunzo hayo yatasaidia wafanyakazi hao ambao wengi wao ni vijana waliofikia umri wa kupevuka kujiepusha na makundi hatarishi yanayoweza kuwashawishi kujiingiza kwenye masuala la mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati.

Rehema Laurent ni mmoja wa wafanyakazi waliopata elimu hiyo, anasema wameyapokea kwa furaha mafunzo hayo na kwamba yanawasaidia kujitambua na hivyo kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kukwamisha ndoto zao maishani.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *