EMAIL US AT info@wotesawa.or.tz
CALL US NOW +255-282-500-599
DONATE NOW

Shirika la WoteSawa limetoa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ugawaji wa taulo za kike za kufua Wilayani Ngara

Date : 7-10 November 2023   Kupitia ufadhili wa @kulczykfoundation,
Shirika la WoteSawa tumeweza
kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibirizi,
Sekondari Keza na Nyakisasa pamoja vikundi vya wasichana vya Keza na
Kashinga. Sambamba na elimu hiyo ilioongozwa na Afisa Afya kutoka
Wilayani Ngara Bi. Mariam Yango, pia tumeweza kugawa taulo za kike za
kufua ( pads) zilizotengenezwa na wahanga wa ukatili katika kazi za
nyumbani kwa wanafunzi hawa na wasichana, tukiamini  taulo (pads) hizi
zitawasaidia wanafunzi na wasichana wengi kujisitiri wawapo katiki
kipindi cha hedhi.
Tunaendalea kutoa shukrani kwa uongozi wa Wilaya ya Ngara kupitia
Mtendaji wa Kata ya Keza na Mkuu wa Shule ya Keza kwa kuweza kuruhusu
shughuli hii kufanyika.
Ahsante pia kwa @kulczykfoundation kwa ufadhili huu na kufanikisha
utengenezwaji wa taulo hizi za kike kufua.

Wotesawa

VIEW ALL POSTS

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *