Shirika la WoteSawa kupitia wawakilishi wake Bi.Mkwaya Manyama na Bi. Ester Petro, tunashiriki mafunzo ya siku tatu kuanzia tarehe 29 hadi 31Mei, yaliyoandaliwa na Shirika la Foundation For Civil Society (FCS), ya usimamizi wa ruzuku (MYG) kwa AZAKI zinazopokea ruzuku za FCS kutekeleza miradi ya maendeleo katika mikoa mbalimbali Tanzania. Lengo ikiwa ni kujifunza na kupeana uzoefu katika kupata matokeo chanya ya mradi mafunzo ya usimamizi wa ruzuku (MYG) Jijini Dodoma.